15 JULAI 2026

15 JULAI 2026

July 15, 2026 · 10 min

About this episode

The episode discusses the role of youth in developing skills in artificial intelligence and their impact on society, featuring an interview with Kalebu Gwalugano from Tanzania.

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya stadi kwa vijana tunamulika jinsi gani vijana waliojiendeleza katika stadi ya akili mnemba au wengine wanaita akili unde, kwa kiingereza Artificial Intelligence au AI, wanarahisisha maisha ya jamii. Na tunamuangazia kijana Kalebu Gwalugano kutoka Tanzania, Muasisi na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Neurotech iliyoanzishwa mwaka 2022. Kijana huyu ni Mhandisi wa AI na akiwa Dar Es Salaam, mji mkuu wa kibiashara wa taifa hilo la Afrika Mashariki, amezungumza na mwenzetu Japhael Jambo. Pia tunakuletea Muhtasariw a habari.Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Stadi za Vijana, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres amesema kuwezesha vijana kufikia uwezo wao kamili kunahitaji uwekezaji mkubwa katika elimu na mafunzo jumuishi yenye ubora. Ametambua mchango wa vijana kote duniani kwamba wanaendelea kutoa mchango mkubwa kama wabunifu, viongozi na mawakala wa mabadiliko katika kujenga jamii zenye usawa, ustahimilivu na maendeleo endelevu hata hivyo mabadiliko ambayo dunia inapitia sasa yakichochewa na maendeleo ya teknolojia za kidijitali, athari za mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuongezeka…

People in this episode

Guest: Kalebu Gwalugano

Topics covered

Keywords

Mentioned in this episode

Organizations: Neurotech

Places: Tanzania, Dar Es Salaam

More episodes of Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Explore listener stats, chart rankings, contacts and more on the Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu podcast page.