16 JULAI 2026

16 JULAI 2026

July 16, 2026 · 10 min

About this episode

The episode discusses the ceasefire in Gaza, the humanitarian situation for Rohingya refugees, and the impact of ongoing conflicts on poverty and health crises.

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Ukanda wa Gaza ambako sitisho la mapigano kati ya Israeli na Palestina lililotiwa Saini tarehe 10 mwezi Oktoba mwaka jana wa 2025 limewezesha wakulima wa eneo hilo kurejea mashambani. Pia tunakuletea Muhtasariw a habari.Mashirika mawili ya Umoja Umoja wa Mataifa lile la Uhamiaji, IOM na la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR kupitia taarifa waliyoitoa kwa pamoja jijini Gneva Uswusi na BangKok Thailand, wameeleza wasiwasi mkubwa kufuatia taarifa kwamba boti mbili zilizokuwa zimebeba zaidi ya watu 500 huenda zimezama katika pwani ya Myanmar katika siku za hivi karibuni. Kwa mujibu wa taarifa za awali, boti hizo mbili ziliondoka mwishoni mwa mwezi Juni kutoka Jimbo la Rakhine nchini Myanmar zikiwa zimewabeba zaidi ya abiria wa jamii ya Rohingya, wakiwemo baadhi waliokuwa wametoka katika kambi za wakimbizi za Cox's Bazar nchini Bangladesh.Zaidi ya watoto milioni 23 wengine zaidi ya wale ambao wako tayari kwenye umaskini duniani wanaweza kutumbukia katika umaskini wa kipato ifikapo mwisho wa mwaka huu wa 2025 kutokana na kuendelea kwa mzozo wa Mashariki ya Kati na athari zake kwa biashara ya kimataifa, kwa mujibu wa ripoti mpya…

Topics covered

Keywords

Mentioned in this episode

Organizations: Umoja wa Mataifa, IOM, UNHCR

Places: Gaza, Myanmar, Bangladesh, Uganda

More episodes of Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Explore listener stats, chart rankings, contacts and more on the Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu podcast page.