
Episodi hii inakuletea mazungumzo ya kina kuhusu mila na tamaduni za Kabila la Wagongwe na mchango wao katika kuhifadhi maliasili.
Episodi hii inakuletea mazungumzo ya kina kuhusu mila, tamaduni na makatazo ya Kabila la Wagongwe lililopo mkoani Katavi na jinsi taratibu hizo zilivyochangia kulinda maliasili na vyanzo vya maji. Mathalani; ilikuwa hairuhusiwi kukata miti iliyokuwa katika vyanzo vya maji kutokaana na imani ya kuwepo kwa nyoka mkubwa wala kuua mnyamapori hadi upewe kibali na pepo au jini Katabi anayepatikana katika Hifadhi ya Taifa Katavi. Sikiliza simulizi hii ya kuvutia katika epsodi ya 13.Eneo: Hifadhi ya Taifa KataviMwongoza kipindi: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine Mbena Wageni:1. Moses Edward Tende ( Mtemi Sigulu) Chifu wa Kabila la Wagongwe.2. Lukas Moses Msaga - Mtoto wa Mtemi Sigulu anayefundishwa kurithi mikoba ya Mtemi Sigulu.3. Askari Uhifadhi Daraja la Pili - Kimori Shiwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ikolojia, Hifadhi ya Taifa Katavi. Endelea kutufuatilia kupitia Platifomu za TANAPA Podcast.TANAPA PODCAST, HIFADHI ZETU, SAUTI YETU.
Host: Catherine Mbena
Guests: Moses Edward Tende, Lukas Moses Msaga, Kimori Shiwa
Organizations: Tanzania National Parks
Places: Hifadhi ya Taifa Katavi, mkoani Katavi, Kabila la Wagongwe
Explore listener stats, chart rankings, contacts and more on the TANAPA PODCAST podcast page.